Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Watanzania waishio nje ya nchi (ughaibuni) hawataweza kupiga kura
wakiwa nje ya nchi kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kutokana na
mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya kufikiwa kwa
hatua hiyo.Akizungumza juzi na baadhi ya Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Peter Kallaghe, yaliyoko Highgate, Kaskazini mwa Jiji la London Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema mambo makuu ambayo yanahitaji kuzingatiwa kabla hawajaweza kupiga kura ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 pamoja na uandikishwaji wa Watanzania wana-Diaspora kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
“Najua suala kubwa ambalo mnatamani kulisikia ni hili la Watanzania kuweza kupiga kura kutokea huku mliko. Hili inawezekana lisifanikiwe wakati huu kwa sababu kuna mambo muhimu ya kuzingatia kubwa likiwa ni marekebisho ya sheria na hili zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.”Alisema Pinda
“Itabidi tuangalie kama mashine za BVR nazo zitapaswa kupelekwa kwenye kila ubalozi ili watu wetu waweze kujiandikisha au itafutwe njia nyingine ya kufanikisha hilo jambo…. lakini watu wa Tume wanaamini kwamba jambo hilo linaweza kufanikiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020,” aliongeza.
Katika hatua nyingine uchaguzi mkuu wa rais,wabunge pamoja na madiwani ili mwananchi aweze kupata haki yake kikatiba ya kupiga kura ni lazima awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Mchakato wa uandishaji kwa kutumia mfumo wa kisasa wa BVR bado unaendelea katika mkoa wa njombe, ikiwa ni mkoa wa kwanza tangu zoezi hilo lianze.
Post a Comment