Uchaguzi wa Rais Sudan kuanza leo
Uchaguzi mkuu nchini Sudan umeanza leo , huku Rais wa sasa Omar Al Bashir akitarajiwa kushinda.
Takriban wapiga kura milioni 13 watakuwa wakimchagua Rais na wabunge 450. Huku vyama vya upinzani vikisusia uchaguzi huu vikidai hautakua huru na wa haki.
Katika vituo vya kupigia kura wapiga kura wachache wamefika huko ilikutekeleza wajibu wao wa kikatiba. Vyama vingi vya upinzani vimesusia uchaguzi huo kutokana na kile vinavyodai kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaoendeshwa na rais Omar al Bashir.
Wagombea 15 wanaoshindana na Bashir kwenye uchaguzi huo inadaiwa kuwa hawana uwezo mkubwa na wengine hata hawajulikani kote nchini Sudan.
Huu ndio utakaokuwa uchaguzi wa kwanza tangu Sudan Kusini ijitenge 2011. Matokeo yanatarajiwa kutangazwa Aprili 27
Labels:
habari
Post a Comment