Katibu Mkuu Chadema Dk Wilbroad Slaa (kushoto) pamoja na Viongozi wakuu wa UKAWA: Prof. Ibrahim Lipumba na James Mbatia. |
Kinyang’anyiro cha Ubunge mwaka 2015 visiwani Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kusimamisha wagombea wake wa nafasi ya ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar, huku Chadema ikiambulia jimbo moja la Kikwajuni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Sheikh, amesema Ukawa wamekubaliana CUF kuchukua majimbo yote isipokuwa katika Jimbo la Kikwajuni watasimamisha mgombea ubunge kutoka Chadema ambaye ni Salum Mwalimu.
Aidha, Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar). Jimbo la Kikwajuni linaunganisha wakazi wa maeneo ya Kikwajuni Juu na Chini, Kisimamajongoo, Kilimani, Miembeni, Magereza na sehemu ya eneo la Michenzani na hadi sasa linamilikiwa na Hamad Yussuf Massauni (CCM), ambaye pia ni mzaliwa wa eneo la Kisimamajongoo.
Hata hivyo watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba Mwalimu amezaliwa na anatoka katika familia yenye makazi katika eneo maarufu la Kisimamajongoo.
Wakazi wa eneo la Kisimamajongoo wanaaminika ni ndugu wa damu hivyo huenda likawa ni moja ya jambo litakalowavutia wananchi wa jimbo hilo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuamua kumpa uongozi Mwalimu.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment