Bw. Said Mirre Siyad akiwa kwenye mahakama ya Nairobi akisubiria kesi |
Katika hali ya kushangaza mtu anaesadikiwa kuwa ni gaidi amekutwa nyumbani mwa Rais Uhuru Kenyatta na alipohojiwa hakuwa na jibu lolote la msingi.
Bw Said Mirre Siyad ambaye alifikishwa mahakamani jana, mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa akuweza kuongea kipi kilimfanya akutwe kwenye maeneo anakoishi Rais bila kibali maalum.
Uchunguzi zaidi juu ya mtuhumiwa unaendelea kwa kufuatilia nyendo zote za simu zinazoingia na kutoka.
Said Mirre Siyad alikuwa ni mmoja ya watuhumiwa nane walifikishwa mahakamani jana kwa kujiusisha na masuala ya kigaidi.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment