![]() |
Rais wa Africa Kusini, Jacob Zuma |
Akihutubia bunge jana alasiri, Rais Zuma alisema mashambulizi hayo yalikiuka haki za kibinadamu kama vile haki ya kuwa hai na kuheshimiwa.
Awali maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamefanya maandamano katika mji wa Durban kulalamikia kile walichotaja kama ukatili dhidi ya Waafrika wengine.
Katika maeneo yanayopakana na Johannesburg, wenye maduka wenye asili ya kutoka Ethiopia, Somalia na maeneo mengine ya Afrika walifunga biashara zao, wakiogopa kuwa mali zao kuporwa.
Post a Comment