![]() |
Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha. |
Daktari ambaye ni shahidi katika kesi ya tuhuma za ubakaji
inayomkabili Mwanamuziki Emmanuel Mbasha ameibua mazito katika kesi hiyo
iliyosikilizwa jana jijini Dar es salaam.
Shahidi huyo ambaye ni daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, ambaye alimfanyia vipimo msichana huyo amedai mahakamani kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili mlalamikaji.
Daktari huyo alidai katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba vipimo alivyomfanyia msichana huyo anayedaiwa kubakwa na Mbasha, havikuonyesha kitu chochote.
Aidha, Dk. Migole alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo. Baada ya kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, akiwa na baadhi ya ndugu wa familia yake, hakwenda bali alitoroka na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.
Baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Flora Mujaya, hawakuweza kusikiliza ushahidi mwingine kutokana na taarifa za msiba wa hakimu mwenzao, zilizofika mahakamani hapo.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya tarehe Mei 23 na 25, mwaka 2014 Bw Mbasha alimbaka binti mwenye umri wa miaka 17, ambaye ni shemeji yake.
Post a Comment