Mwanasheria wa Chama cha Chadema Tundu Lissu . |
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu anatarajia kuwahutubia wananchi katika manispaa ya Dodoma siku ya Jumatano tarehe tatu ya wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na kutangazwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma na Viunga vyake kwa kutumia gari la matangazo lenye vipaza sauti imebainisha kuwa Tundu Lissu atazungumza na wananchi wa Manispaa ya Dodoma katika uwanja wa Barafu.
Taarifa hiyo haijazungumzia zaidi masuala ambayo mwanasheria huyo wa Chadema atayazungumzia.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment