Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama jana. |
Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere naye ametangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama jana.
Akizungumza na Wananchi Makongoro, amesema anatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo kutokana na kukerwa sana na rushwa, kwa kuwa inasababisha Watanzania wengi kupoteza haki zao.
Pia Makongoro amesema anatambua kuwa kuna makundi ndani ya CCM. Akipata nafasi ya urais na baadaye kuwa mwenyekiti wa CCM atayamaliza na wote tutabaki kitu kimoja.
Amesisitiza kuwa ataboresha hali ya majeshi ya Tanzania, pamoja na wanafunzi elimu ya juu kupata mikopo kwa wakati.
Amesisitiza kuwa Rais Kikwete, amefanya kazi nzuri katika kipindi cha uongozi wake, lakini kuna watu wanamhujumu ili aonekane hafanyi kazi.
Makongoro anakuwa mwanasiasa wa tano kutangaza nia ya kutaka kuwania urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, wengine ni Luanga Mpina,Edward Lowassa, Steven Wassira, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu huku wengine wakijitokeza tena leo.
Post a Comment