vote

Mwandosya atangaza nia ya kugombea Urais, alia na wanaojilimbikizia mali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya akitangaza nia ya kugombea Urais.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya ametangaza kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo eneo la Soko Matola jijini Mbeya.

Akizungumza  wakati akitangaza nia Prof. Mwandosya amesema kamwe hawezi kuwavumilia mafisadi na walarushwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais  atapambana na mafisadi, walarushwa na wanaofanya udhalimu kwa kujikusanyia mali kwa njia isiyo ya haki.

Akibainisha vipaumbele vyake amesema,   moja kati ya vipaumbele alivyonavyo ni  kuwa na viongozi waadilifu wenye uchungu wa rasilimali za Watanzania ambao hawako tayari kujilimbikizia mali.

Amesema wapo viongozi wengi waliojitokeza kuwania nafasi hiyo huku wakimwaga fedha jambo ambalo halipaswi kufanywa na viongozi wanaotarajia kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu.

Amesisitiza kuwa  wakati wa Mwalimu Nyerere rushwa ilikuwa ni adui wa haki,leo hii rushwa iko nje nje kama njugu, wanapotoa hela zao chukueni,lakini msiwaunge mkono hawafai kuongoza nchi.

Chanzo: Hivi Sasa
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog