vote

Tazama list ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu 2015

Msajili Msaidizi Ndugu Sisty Nyahoza kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.



Vyama  vya  siasa 22  vitashiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu utakaofanyika tarehe 25.

Kwa mujibu wa  taarifa iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa jana Dar es Salaam na kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza, imetaja idadi hiyo ya vyama vyama hivyo, ambavyo ni vyenye usajili wa kudumu kuwa ni ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Union for Multiparty Democracy (UMD) na Chama cha NCCR-Mageuzi.

Vingine ni National League for Democracy (NLD), UnitedPeoples’ Democratic Party (UPDP), National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party (TADEA), Tanzania Labour Party (TLP) na United Democratic Party (UDP).

Aidha vyama vingine ni Demokrasia Makini (Makini), Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), Democratic Party (DP), African Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) na Jahazi Asilia.

Kwa upande mwingine kuna chama cha Sauti ya Umma (SAU), Tanzania Farmers Party (AFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC), Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) na Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo).
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog