|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal
katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015
katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu
ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya
ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akutana na kufanya mazungumzo
na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika
katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika
siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete yupo nchini
Algeria kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana na na kufanya mazungumzo
na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Bw. Abdelazizi Bouteflika
katika Ikulu ya hiyo jijini Algiers.
Aidha, Katika ziara hiyo Rais Kikwete ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernad Membe.
Rais Kikwete atakuwa nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku ya tatu.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment