vote

Lowassa na Haji Duni Kupeperusha Bendera Ukawa

Mgombea Mwenza Haji Duni, (kushoto) na Mgombea urais Edward Lowassa.







Mkutano Mkuu wa Chadema kwa pamoja umempitisha Mwanasiasa Edward Lowassa kama mgombea Urais na Juma Haji Duni kuwa mgombea Mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 oktoba 2015.


Katika upigaji kura  Kanda zote zimepiga  kura ya NDIYO kwa Mh. Edward Lowassa  na hakuna kanda iliyosema HAPANA, huku wakishangilia kwa nguvu.

Kanda ya Kaskazini, Kanda ya kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kusini na nyingine zote pia zimepiga kura ya NDIYO kwa Juma Haji Duni kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi nkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kufuatia matokeo hayo Mwanasiasa Edward Lowassa  atapambana na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na wagombea wengine akiwemo Mchungaji Christopher  Mtikila wa chama cha DP aliyechukua fomu ya urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog