Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara. |
Msafara wa jeshi la Polisi wakimsindikiza mwekezaji Dangote mkoani Mtwara. |
Wananchi wakiangalia msafara wa mwekezaji Dangote. |
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote. |
Kiwanda cha Simenti kinachojengwa mkoani Mtwara chini mwekezaji Dangote. |
Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dangote amewasili mkoani Mtwara kwa lengo la kukagua ujenzi wa kiwanda chake cha Simenti.
Aidha, katika ziara yake mkoani Mtwara pia amekagua eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Mamia ya wananchi kijijini hapo wamejitokeza kumlaki bilionea huyo ambapo wamedai kuwa uwekezaji wake utasaidia kuinua uchumi kwa wananchi mkoani mtwara kwa kuwa wanategemea kupata ajira kwenye uwekezaji huo.
Kiwanda hicho kinategemewa kutoa ajira zaidi ya 5000 pindi kitakapoanza uzalishaji
Wanakijiji kinapojengwa kiwanda hicho wamempa Dangote mgao wa eneo la hekari 2,500 la nchi kavu na bahari ili ajenge bandari, makazi ya kudumu katika kijiji cha Msijute pamoja na kutoa eneo kwa ajili ya makazi ya balozi wa Nigeria mkoani Mtwara.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment