Baadhi ya raia wa Afrika Kusini wanao watimua wageni nchini humo. |
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la wenyeji kuwatimua wageni nchini humo.
Aidha, mikutano mikubwa imeandaliwa katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni mnamo mwaka 2008.
Hata hivyo makundi ya kiusalama yanafanya misako katika majumba ya makazi katika mji wa Alexandra mjini Johannesburg, sehemu ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.
Katika hatua nyingine nchi mbalimbali zimeibuka na kulaani vikali vitendo vinavyofanywa na raia wa Afrika kusini kuwatimua wageni kwa madai kwamba wanachukua nafasi zao za kazi. Nchi hizo ni pamoja na Nigeria na Malawi huku Tanzania ikiwa katika harakati za kuwarejesha raia wake nyumbani.
Post a Comment